USHINDI WA MABAO 7-1 WAIPA JEURI LIVERPOOL

BAADA ya kichapo cha mabao 7-1 walichokitoa Liverpool kwa Rangers katika Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi kimemfanya Jurgen Klopp aamini kwamba watakuwa wanajiamini kuelekea mchezo wao dhidi ya Man City.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumapili unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa mpira kutokana na ushindani wa timu hizo mbili.

Ni mabao matatu ambayo yalifungwa na staa wa timu hiyo Mo Salah na jingine lilifungwa na Darwin Nunez, mabao mawili mali ya Roberto Firmino na moja mtupiaji ni Harvey Elliott.

Klopp amesema kuwa ushindi ambao wameupata umetokana na mchezo bora wa wachezaji wake Uwanja wa Ibrox ambapo timu hizo zipo kundi C.

“Mabao yalikuwa ni mali sanana tulikuwa na mazungumzo mazuri wakati wa mapumziko. Hii inabadilika kabisa mudi ni tofauti kabisa lakini wote tunajua tunamkaribisha nani Jumapili.

“Hatutaki kukuza mambo lakini timu bora zaidi duniani kwa sasa inakuja Anfield Jumapili, tutaona tutakachokifanya,” amesema.