TIMU YA TAIFA YA TANZANIA YAANZA KOMBE LA DUNIA KWA MAUMIVU

TIMU ya taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 17 leo Oktoba 12,2022 imepoteza mchezo wa kwanza kwenye Kombe la Dunia dhidi ya Japan.

Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru umesoma Japan 4-0 Tanzania.

Shiragaki alifunga bao la ufunguzi kipindi cha kwanza na kufanya dakika 45 kukamilika Japan wakiongoza kwa bao moja.

Mvua ya mabao ilitokea kipindi cha pili ambapo ni jumla ya mabao matatu Tanzania ilifungwa.

Ni Hamura alifunga dakika ya 67, Isojoha dakika ya 75 na Tamikawa alifunga bao la nne dakika ya 80.

Makosa ya safu ya ulinzi ya Tanzania yalikuwa ni chanzo cha mabao hayo manne ambapo dakika 90 zilikamilika wakiwapungufu baada ya Neema Kinega kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 20 kwa kuwa alionyeshwa kadi mbili za njano.

Licha ya kufungwa pongezi kwa kipa namba moja wa Tanzania Zulfa Makau ambaye aliokoa michomo minne ya maana ilikuwa dakika ya 45,45,69 na 88.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Tanzania kucheza Kombe la Dunia jambo ambalo linakuwa rekodi ya muda wote .