KINDA BRIGHTON ASTAAFU SOKA KUTOKANA NA MATATIZO YA MOYO

KIUNGO wa Brighton Mzambia, Enock Mwepu amelazimika kustaafu soka akiwa na miaka 24 baada ya kubainika kuwa ana matatizo ya moyo.

Mwepu alijiunga na Brighton akitokea Red Bul Salzburg msimu uliopita kwa dau la pauni milioni 18 na msimu huu amecheza mechi sita za Premier.

Tatizo lake lilianza kubainika wakati wa mapumziko ya timu za taifa hivi karibuni akiwa na timu ya taifa ya Zambia kwani alilazimika kupelekwa hospitali walipoenda kucheza nchini Mali alivyorudi Brighton alifanyiwa vipimo zaidi.

Baada ya vipimo hivyo ilionesha kuwa ana tatizo katika moyo wake hivyo alishauriwa kama anataka kuwa salama ni bora akaachana na soka.

Mwenyekiti wa Klabu ya Brighton, Tony Bloom alitoa taarifa kuhusu kiungo huyo akisema:”Wote tumeshtushwa na taarifa ya Enock. Yeye pamoja na familia yake wamekuwa katika wakati mgumu lakini imekuwa mapema kwa umri wake akiwa bado mdogo kulazimika kustaafu soka,”.