FIFA YAITAKA YANGA ILIPE FAINI KWA EYMAEL

IMEELEZWA kuwa Yanga wameambiwa wamlipe Luc Eymael aliyekuwa kocha wa timu hiyo msimu wa 2020 kiasi cha dola milioni 152 za kimarekani.

Taarifa kutoka Shirikisho la Soka Kimataifa, (FIFA) imeeleza kuwa Yanga wamepewa siku 45 kulipa fedha hizo.

Ikiwa watakwama kukamilisha shauri hiyo kwa muda wa siku 45 watapewa adhabu ya kufungiwa kufanya usajili kwenye madirisha matatu ya usajili.

Sababu ya Yanga kupewa adhabu hiyo ni kufanya kumfuta kazi kocha huyo bila kufuata utaratibu.

Yanga iliachana na Eymael Julai 2020 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuonyesha vitendo vya kiubaguzi jambo ambalo sio sawa.

Uongozi wa Yanga ulipotafutwa uzungumzie suala hili ulibainisha kuwa kwa sasa wapo kwenye hesabu za mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal.