WAKUBWA NA WAONYESHE UKUBWA KIMATAIFA

    JAMBO dogo likibadilika kwenye kitu lazima kila mmoja atakuwa na makasiriko kwenye moyo wake akiamini kwama anaonewa ama akiamini hakustahili kufanyiwa hilo.

    Ukweli ni kwamba kama hautakubali mabadiliko yatokee kwenye maisha wewe umekata tamaa na hatukati kuendelea kupambana na maisha.

    Pale inapotokea jambo jipya na geni kwako ni fursa ya kujifunza na kuamini akili yako kuwa unaweza kufanya hata katika mazingira ya aina gani.

    Iwe jua ama mvua hiyo ni kauli mbiu inayotumiwa na Yanga hii ni kubwa na inapaswa kuhesjhimiwa na kila mmoja kwa kuwa hili ni jambo geni kwa mashabiki na sasa wanataka kuona namna gani itafanya kazi.

    Azam FC wao wana jambo lao wakiwa chimbo pale Azam Complex kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kimataifa muhimu kuwa makini kwa ajili ya mechi zijazo.

    Kwa Simba wao wanasema hawazuiliki na hakuna wa kuwazuia kwa namna ambavyo wameamua kuja na jambo lao ni sawa kwa kuwa yote ni mapya.

    Imekuwa ni nadra sana kwa wengi kuishi katika yale wanayoyasema mdomoni kwenye uhalisia kutokana na kuhofia kufanya mambo mapya.

    Ikiwa kwa sasa bado kuna watu wanajadili kuhusu nani ataanzia nyumbani na nani ataanzia ugenini kimataifa hilo sio la msingi muhimu kwanza  ni matokeo.

    Unaweza ukaanzia ugenini ukafungwa na ukaja nyumbani ukafungwa pia na ukaanzia nyumbani ukashinda kisha ukaaenda ugenini ukashinda, inawezekana.

    Maisha ya mpira hayana kanuni maalumu wala hayana mshindi maalumu kila mmoja ni mshindi kwenye maisha ya mpira ikiwa atakubali mabadiliko ambayo yatatokea.

    Hakuna anayeweza kutoa majibu kwa sasa kwamba nani ana nafasi ya kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ama Simba pamoja na nafasi ya Azam FC kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

    Ambacho kinaonekana kwa sasa ni kila kiongozi kuweka tambo nyingi na maneno kwamba wao ni wakubwa na wanaweza kufanya mambo makubwa.

    Haya ni maneno ambayo yasipofanyiwa kazi yatakuja kuwa hukumu wao wenyewe baadaye hivyo ni muhimu kuwekeza nguvu kwenye ukweli na kufanya yote kwa vitendo.

    Muda ambao umebaki kwa sasa hautoshi kuweza kuweka maneno mengi na badala yake ni muda wa kazi kwa vitendo.

    Hakika ikiwa maandalizi yatakuwa bora na wachezaji watafanya kazi kubwa kwenye kusaka ushindi uwanjani itawapa matokeo mazuri.

    Watanzania wanasubiri kuona kila timu inafanya vizuri kwenye mechi zote za kimataifa na inawezekana ikiwa kila haya mambo mapya yanayofanyika kwenye sera yakawa kwenye vitendo.

    Wapo wachezaji wapya ambao wamesajiliwa na timu zao nao pia wanaanza kuishi kwenye mazingira mapya ni lazima kukubali kwamba ugeni wao isiwe sababu ya kushindwa kufanya vizuri.

    Kila kitu kinawezekana na muda ni sasa kukamilisha yale mambo yote yaliyopangwa kwa vitendo na kimataifa kazi ikafanyike kwelikweli nyumbani ama ugenini.

    Previous articleSAUTI:MILIONI 300 ZATUMIKA UJENZI WA UWANJA SIMBA
    Next articleMERIDIANBET SLOTI, SASA KWENYE MADUKA YA MERIDIANBET