JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema ushindi ambao wameupata kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji umetokana na kazi kubwa ya wachezaji wakeo uwanjani.
Baada ya dakika 90, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 3-0 Dodoma Jiji na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 13 na kuongoza ligi.
Bao la ufunguzi lilifungwa na Abdallah Shaibu,’Ninja’ kwenye harakati za kuokoa hatari dakika ya 4 kisha bao la pili likafungwa na Moses Phiri dakika ya 45.
Kipindi cha pili ni bao moja lilifungwa na Habib Kyombo ambaye alikuwa anasoma mchezo akiwa benchi alifunga bao hilo dakika ya 85.
Masod Djuma, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji amesema kuwa wameshindwa kupata matokeo kutokana na kukosa utulivu