USIKU kabisa Chelsea wakiwa ugenini wamepeleka maumivu kwa Crystal Palace kupitia kwa Conor Gallagger dakika ya 90.
Bao hilo lilifanya ubao wa Uwanja wa Selhurst Park kusoma, Crystal Palace 1-2 Chelsea.
Bao la mapema kwa Crystal Palace lilijazwa kimiani na Odsonne Edouard dakika ya 9 liliwekwa usawa na Pierre Emerick Aubameyang dakika ya 38.
Chelsea inafikisha pointi 13 nafasi ya tano na Crystal nafasi ya 17 na pointi ni 6 kibindoni.