AZAM FC KUIKABILI PRISONS, RUVU SHOOTING YAICHAPA COASTAL UNION

MCHEZO mmoja wa Ligi Kuu Bara leo unatarajiwa kuchezwa, Uwanja wa Sokoine ambapo itakuwa ni kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Azam FC.

Wageni Azam FC, jana waliwasili Mbeya na walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo miongoni mwao ni pamoja na nyota Agrey Morris.

Idd Nado ambaye alikuwa nje kwa muda kutokana na kutokuwa fiti ni miongoni mwa nyota ambao wamerejea katika kikosi hicho.

Jana ni mechi mbili za ligi zilichezwa ilikuwa Ruvu Shooting 2-1 Coastal Union huku mabao yakifungwa na Rashid Juma huyu alitupia mabao mawili dakika ya 36 na 60 huku lile la Coastal Union likifungwa na Vincent Abobakar dakika ya 8.

Dodoma Jiji imepata ushindi wake wa kwanza kwa kuichapa Geita Gold bao 1-0 huku mtupiaji akiwa ni Collins Opare dakika ya 29.