AJIBU AACHWA DAR AZAM IKIWAFUATA TANZANIA PRISONS

LEO  Septemba 29,2022 msafara wa Azam FC ukitarajiwa kuelekea Mbeya kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons, kiungo wao Ibrahim Ajibu ni miongoni mwa watakaoaki Dar.

Azam FC inarejea kwa mara nyingine Mbeya kwenye mchezo wa ligi baada ya ule uliopita kucheza dhidi ya Mbeya City na kuambulia ushindi wa bao 1-0.

Sababu ambazo zinamfanya nyota huyo ambaye kandarasi yake inakaribia kugota mwisho zimeelezwa kuwa ni za kiufundi.

Orodha ya mastaa wengine ambao watakosekana kwenye mchezo huo iliyotolewa na Azam hii hapa:-

Ali Ahamada – majukumu ya kitaifa
Wilbol Maseke – majeruhi
Abdallah Kheri Sebo – sababu za kiufundi
Issa Ndala – majeruhi
Kenneth Muguna – majeruhi
Ismail Aziz Kader – sababu za kiufundi
Abdul Hamis Sopu – sababu za kiufundi
Rodgers Kola – adhabu

Hivyo ni mastaa 9 wanatarajiwa kuikosa Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.