Home Sports KOCHA AZAM FC ATAJA FAIDA MCHEZO DHIDI YA TP MAZEMBE

KOCHA AZAM FC ATAJA FAIDA MCHEZO DHIDI YA TP MAZEMBE

KOCHA Mkuu wa Azam FC Denis Jean Lavagne ameweka wazi kuwa mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe utampa nafasi ya kuwajua wachezaji wake kwa ukaribu.

Wachezaji 20 wa Azam FC wanatarajiwa kukwea pipa leo kuelekea Zambia kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya TP Mazembe.

“Mazoezi ni mazuri na kila mchezaji anaonyesha uwezo weke hivyo mchezo wetu dhidi ya TP Mazembe utanipa nafasi ya kuweza kuwaona zaidi wachezaji ambao sikupata nafasi ya kuwaona kweye mchezo wetu wa kwanza.

“Pia mchezo huo utatumika kwa ajili ya wachezaji wengine ambao hawakupata nafasi ya kuweza kuanza kwenye mchezo wetu ambao tulicheza Mbeya,” amesema.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Ijumaa na utarushwa mubashara Azam TV.

Mchezo wa kwanza wa Lavagne alishuhudia timu hiyo ikishinda bao 1-0 dhidi ya Meya City na mtupiaji akiwa ni Idris Mbombo dakika ya 60.

Previous articleKWA MIPANGO HII YANGA INATOBOA CAF, SIMBA HAKUNA KULAZA DAMU
Next articleVIDEO: SAKHO APEWA NENO LAKE, WAPINZANI WA SIMBA SIO WAKUBEZA