>

MAYELE MTAMBO WA MABAO YANGA

NDANI ya Yanga ni Fiston Mayele anaongoza kwa kutupia mabao akiwa nayo matatu, aliwatungua Polisi Tanzania, Coastal Union na Mtibwa Sugar.

Msimu uliopita Mayele alitupia mabao 16 na pasi nne za mabao kinara alikuwa ni George Mpole wa Geita Gold alitupia mabao 17.

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kila mchezaji anahitaji kufanya vizuri jambo ambalo linawafanya wazidi kuendelea kupambana ndani ya ligi na mechi za kimataifa.

Septemba 17,2022 Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Zalan FC kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye hatua ya awali Mayele ametupia mabao matatu na kusepa na mpira wake huku Feisal Salum yeye akitupia bao moja waliposhinda mabao 4-0