RELLIATS Lusajo ni namba moja kwa utupiaji Bongo akiwa ametupia mabao manne na bao lake la nne aliwatungua Ruvu Shooting, mchezo uliochezwa Uwanjawa Majaliwa.
Kwenye mchezo huo ambao ni wa kwanza kwa Namungo kucheza Uwanja wa Majaliwa msimu wa 2022/23 kutokana na kufanyiwa marekebisho walijitokeza mashabiki wengi na burudani ilikuwa kubwa.
Bao pekee la Lusajo lilifungwa dakika ya 82 zikiwa zimesalia dakika 8 mchezo kukamilika Uwanja wa Majaliwa.
Lusajo anakuwa mzawa wa kwanza kuwa kwenye mwendo wa kufunga kwenye mechi tatu mfululizo kwa kuwa aliwafunga Mtibwa Sugar mabao mawili, Ihefu bao moja na jana kawatungua Ruvu bao moja.
Mwingine ambaye amefanikiwa kutupia mabao kwenye mechi tatu mfululizo ni Moses Phiri wa Simba.