SIMBA KUWASILI DAR LEO

KIKOSI cha Simba leo Septemba 11,2022 kinatarajiwa kuwasili Dar kikitokea Malawi ambapo kilikuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ulikuwa ni mhezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets, uliochezwa Septemba 10,2022 na ubao wa Bingu ulisoma Big Bullets 0-2 Simba.

Mabao ya Moses Phiri na John Bocco yalitosha kuwapa ushindi kwenye mchezo huo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa baada ya kumaliza mchezo wao maandalizi ya kurejea Dar yalianza.

“Baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wetu dhidi ya Big Bullets, leo wachezaji wamefanya mazoezi ya kujiweka sawa mwili kabla ya kuanza safari ya kurudi Dar.

“Tukirejea wachezaji watapewa mapumziko mafupi na Jumatatu watawasili kambini na kuanza mazoezi kwenye Uwanja wa Bunju kisha Jumanne tutaelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons,” amesema.