BAO pekee la ushindi kwa Real Sociedad dhidi ya Manchester United lilipachikwa dakika ya 59 kwa mkwaju wa penalti na mtupiaji alikuwa ni Brains Mendez kwenye mchezo wa Europa, Uwanja wa Old Trafford.
Kwenye mchezo huo ni mashuti 15 yalipigwa kuelekea lango la Real Sociedad huku matatu pekee yakilenga lango.
Real Sociedad wao walipiga jumla ya mashuti 7 huku mashuti matatu yakilenga lango Uwanja wa Old Traford.
Katika kundi E, Sherif wanaongoza kundi huku Real Sociedad wao wakiwa nafasi ya pili wote wakiwa na pointi tatu wakitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungana.