Home Sports ORODHA YA MASTAA KUTOKA DR CONGO YATAWALA BONGO

ORODHA YA MASTAA KUTOKA DR CONGO YATAWALA BONGO

LIGI Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23 imeanza kwa ushindani mkubwa huku kila timu zikikamilisha usajili wao kwa kile ambacho walikuwa wanahitaji.

Nyota wapya wakigeni wapo ikiwa ni pamoja na kutoka Uganda, Burundi, Rwanda lakini nyota kutoka DR Congo wametawala soka la Bongo.

Hapa tunakuletea baadhi ya nyota wakigeni kutoka DR Congo ambao wanakipiga kwenye ligi namna hii:-

 Djuma Shaban ni beki wa Yanga yeye ni raia wa DR Congo, mbali na Djuma yupo Fiston Mayele, Joyce Lomalisa, Yannick Bangala, Tuisila Kisinda, Jesus Moloko na Heritier Makambo hawa wapo Yanga.

Wengine ni pamoja na Henock Inonga yupo zake ndani ya Simba, Idris Mbombo ni mali ya Azam FC, Carno iemes wa Singida Big Stars, Mwana Kibuta na Randy Bangala wanakipiga ndani ya Dodoma Jiji.

Ukiwagusa Coastal Union wanaye Mbaya Kayembe na Eric Yema yupo Geita Gold, Alidor Kayembe mali ya Namungo FC, Pascal Kitenge ni Mtibwa Sugar na Papy yupo Ihefu zote zinashiriki Ligi Kuu Bara.

Previous articleVIDEO:SHABIKI SIMBA AWAZUNGUMZIA INONGA,BANGALA,MZUNGU
Next articleMWAKINYO ATAJA SABABU ZA KUPIGWA TKO