KOCHA MAN U AKIRI ARSENAL NI WAGUMU

 ERIC ten Hag, Kocha Mkuu wa Manchester United ameweka wazi kuwa atakabiliana na wapnzani wao Arsenal ambao ni kipimo sahihi kwake kutokana na ubora wa wapinzani wao hao kwa sasa.

Man United inatarajiwa kuvaana na Arsenal leo Septemba 4,2022 Uwanja wa Old Trafford ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu England.

Arsenal imeanza msimu wa 2022/23 kwa kasi imecheza mechi tano mfululizo na kushinda zote ikiwatungua Crystal Palace, Leicester City, Bournemouth, Fulham na Aston Villa na United wao wameshinda mechi tatu na kupoteza mbili.

Kocha huyo amesema:”Nimeona Arsenal ni timu ngumu hilo liko wazi walianza msimu vizuri na kocha wao ameisuka timu vizuri wakiwa na falsafa bora ndiyo maana mambo yanaenda vizuri,” .

Mikel Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema:”Sishangai kuona Manchester United imeanza kurudi baada ya kuanza kufanya vibaya wanawachezaji wazuri lakini lazima tupambane nao kwa bidii,”.