STAA wa Klabu ya Real Madrid, Karim Benzema amebainisha kuwa nyota Cristiano Ronaldo amefanya kazi kubwa kumsaidia yeye kuwa bora baada ya kuondoka hapo na kumuachia majukumu.
Benzema na Ronaldo walicheza pamoja Real Madrid kuanzia 2009 mpaka 2018 kwa mafanikio makubwa ndani ya La Liga.
Mpaka Ronaldo anaondoka Madrid alikuwa ametupia mabao zaidi ya 420 na kuwa kinara katika historia ya klabu hiyo na sasa Benzema ni namba mbili ametupia mabao 324.
Benzema amesema:”Cristiano amenisaidia sana tukiwa tunacheza pamoja alikuwa na majukumu yake na mimi nilikuwa nina majukumu yangu, alipoondoka ilibidi nipige hatua kwa kufunga mabao mengi zaidi na soka langu linaendelea kubaki vilevile,” amesema.
Nyota huyo ana miaka 34 kwa sasa ila amekuwa na uwezo mkubwa ndani ya uwanja katika kutimiza majukumu.