RASMI Geita Gold FC imemtambulisha nyota wao mpya Said Ntibanzokiza kuwa ni mali yao kwa msimu wa 2022/23.
Anaibuka ndani ya Geita Gold akiwa ni mchezaji huru baada ya dili lake na Yanga kugota ukingoni mwishoni mwa msimu wa 2021/22.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Geita Gold imeeleza kuwa ni dili la mwaka mmoja amesaini nyota huyo.
Taarifa hiyo imeeleza:” Geita Gold FC tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumefikia makubaliano na kiungo mshambuliaji Said Ntibanzokiza kuitumikia klabu yetu kwa mkataba wa mwaka mmoja.
“Godfather wa Bujumbula anakuja kuongeza nguvu katika idara ya ushambuliaji,”.
Timu hiyo inawakalisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ambapo itakuwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika inatarajiwa kuanza ugenini kwa mchezo wao dhidi ya Hilal Alsahil ya Sudan.