IKIWA nchini Sudan kwa ajili ya mashindano maalumu waliyoalikwa na Al Hilal, mastaa 10 wa Simba wanatarajia kukosekana kwenye mechi hizo.
Tyari Maki ameongoza kikosi cha Simba kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Asante Kotoko ambapo walishinda mabao 4-2 kesho Agosti 31 ni mchezo mwingine dhidi ya Al Hilal ambao ni wenyeji.
Ni nyota 9 ambao wapo kwenye timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ikiwa ni Aishi Manula, Beno Kakolanya,Shomari Kapombe,Mohamed Hussein, Kenned Juma, Jonas Mkude,Mzamiru Yassin,Kibu Dennis na Habib Kyombo pia kiraka Erasto Nyoni hayupo fiti.
Seleman Matola, koca msaidizi wa Simba amesema: “Wachezaji 9 wapo kwenye timu ya taifa hawa wana majukumu na tutawakosa pia Erasto Nyoni huyu yeye anasumbuliwa na Malaria.
“Kwa wachezaji ambao wapo wote wapo tayari na tunakwenda kwenye mashindano haya kucheza kwa umakini ili kupata matoke hatutayachukua mashindano haya kwa hali ya kawaida tunaheshimu mashindano haya,” amesema.