PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amebainisha kuwa kiungo Bernardo Silva hatajiunga na Barcelona kwa sababu mpaka sasa hakuna mbadala wake.
Kocha huyo amebainisha kuwa mchezaji huyo ni kiungo wa kipekee ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England hivyo timu hiyo inakutana na kisiki kupata saini ya mwamba Silva.
Nyota Silva alikuwa kwenye hesabu za Barcelona inayoshiriki La Liga ili aweze kujiunga nayo kwa ajili ya kupata changamoto mpya.
Tayari Barcelona imefanikiwa kuinasa saini ya Frank Kesie, Robert Lewandowski, Raphinha na Jules Kounde.
Guardiola amesema:”Bernardo Silva hatajiunga na Barcelona atabaki hapa Manchester City hilo ninaomba lieleweke kabisa.
“Bernado hana mbadala na hakuna wa kufanana naye amekuwa akitupa vitu vingi na tofauti,” amesema.