MANCHESTER United inatajwa kuwania saini ya mshambuliaji wa Barcelona, Memphis Depay ili kuwanaye ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu England.
Wanatajwa kuweka mezani kiasi ch pauni 8.4 milioni ili kuweza kumnasa mshambuliaji huyo.
Msimu wa 2021/22 nyota huyo ndani ya La Liga alitupia mabao 12 akiwa ni kinara wa utupiaji ndani ya Barcelona.
Awali nyota huyo aliwahi kuichezea United msimu wa 2015 ila alikwama kutamba katika kikosi hicho na alitimkia Lyon kabla ya kutua Barca.
Ripoti zinaeleza kuwa United wamekuwa wakifuatilia dili lake kimyakimya kwa nyota huyo ambaye Barcelona inataka kumuuuza.