ARSENAL WAPINDUA MEZA NA KUJIIMARISHA JUU

UPINDUAJI wa meza mbele ya Fulham ambao walitangulia kupachika bao dakika ya 56 kupitia kwa Aleksandar Mitrovic unawafanya Arsenal kuanza kwa kasi msimu wa 2022/23.

Dakika 8 zilitosha kwa Klabu ya Arsenal inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta kufanya yao kwa kuanza kufunga mabao yao.

Ni Mardtin Odegaard aliweza kuweka usawa ilikuwa dakika ya 64 ya mchezo huo na kuwapa nguvu vijana hao kuendelea kupambana.

Bao la ushindi lilifungwa na Gabriel Jesus dakika ya 85 na kuifanya Arsenal kuongoza Ligi Kuu England ikiwa na pointi 12 huku Fulham ikiwa nafasi ya 11.