MAN UNITED YAICHAPA LIVERPOOL

 MANCHESTER United imesepa na pointi tatu mazima mbele ya Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Old Traford.

Mabao ya Jadon Sancho dakika ya 16 na Marcus Rashford yalitosha kuipa pointi tatu muhimu timu hiyo.

Bao la Liverpool lilifungwa na Mohamed Salah dakika ya 81.

Rekodi zinaonyesha kuwa United ilipiga jumla ya mashuti 12 huku Liverpool wakipiga mashuti 17.

Ni mashuti manne yaliweza kulenga lango na mashuti matano kwa Liverpool yalilenga lango.

United inafikisha pointi tatu baada ya kucheza mechi tatu ikiwa ni ushindi wake wa kwanza huku Liverpool ikibakiwa na pointi mbili baada ya kucheza mechi tatu.