NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa kwa sasa hawana mpango wa kuweza kumsajili mchezaji mwingine wa kigeni kama ambavyo imekuwa ikielezwa.
Jina la nyota Cesar Manzoki ambaye ni mali ya Vipers SC ya Uganda limekuwa likitajwa kuweza kumalizana na Yanga kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo msimu wa 2022/23.
Pia mshambuliaji huyo amekuwa akitajwa kuingia rada za Simba ambapo hivi karibuni aliweka wazi kwamba amemalizana na mabosi wa Msimbazi ni suala la muda kuweza kutambulishwa.
KochA Nabi amesema:”Kuhusu usajili wa wachezaji wakigeni kwa sasa hapa hakuna kwani tumeshamaliza kazi na hakuna jambo lingine ambalo tunafikiria zaidi ya kuweza kupata matokeo kwenye mechi zetu.
“Kuhusu Manzoki kuja Yanga hapana, labda kama kuna timu nyingine ambayo inamuhitaji kwani hapa kwetu wachezaji wakigeni wametosha,” amesema.
Miongoni mwa wachezaji wakigeni ambao wapo ndani ya Yanga ni pamoja na Bernard Morrison, Aziz KI, Jesus Moloko na Gael Bigirimana.