KANE AWEKA REKODI LIGI KUU ENGLAND

 MSHAMBULIAJI wa Tottenham, Harry Kane ameweka rekodi yake wakati timu hiyo ikishinda bao 1-0 dhidi ya Wolves kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana.

Kane alivunja rekodi ya Aguero kwa kufikisha mabao 185 na kuwa mchezaji ambaye amefunga mabao mengi akiwa na timu moja ndani ya Ligi Kuu England.

Nyota huyo amebeba tuzo ya ufungaji bora mara tatu katika Ligi Kuu England ambayo ni ngumu na ina ushindani mkubwa.

Aguero wakati anacheza ndani ya Man City kuanzia 2011-2021 aliweza kutupia jumla ya mabao 184 kwenye ligi hiyo.

Kane amecheza ndani ya kikosi hicho tangu mwaka 2009 akianzia kikosi cha vijana na walishinda mchezo huo  wakiwa Uwanja wa Totttenham.