MZUNGU WA SIMBA ATUPIA MBELE YA KAGERA SUGAR

SIMBA imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mabao ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Zoran Maki yamefungwa na Moses Phiri dakika ya 42 na bao la pili lilifungwa na Dejan dk ya 81.

Simba inafikisha pointi 6 kibindoni baada ya kucheza mechi mbili kwa msimu wa 2022/23 huku kipa namba moja Aishi Manula akiwa amecheza mechi yake ya pili mfululizo bila kufungwa.

Dejan amefunga bao lake la kwanza akiwa na Simba ikiwa ni ingizo jipya katika kikosi cha Simba.

Mashabiki wa Simba baada ya bao la Dejan kufungwa walikuwa wakishangilia kwa nguvu wakisema mlete mzungu.