Home Uncategorized IJUE SABABU YA MASHINDANO MAPYA AFRIKA

IJUE SABABU YA MASHINDANO MAPYA AFRIKA

RAISI wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika, Patrice Motsepe ametangaza kuanzishwa kwa mashindano mapya ya vilabu Afrika yatakayo julikana kama “CAF Super League” alipokuwa akizungumza katika mkutano mkuu wa CAF uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha nchini Tanzania.

Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Agosti,2023 ikihusisha timu 24. Malengo makubwa ya michuano hiyo ni kusaidia timu za Afrika kiuchumi ili kuweza kuendana na kasi ya ukuaji wa mchezo wa mpira wa miguu na kuweza kushindana na timu kubwa nje ya Afrika.

Motsepe amesema “Ukiwa mchezaji wa mpira unakuwa na muda mchache wa kufanya kazi kwahiyo inabidi upate pesa nyingi ili baada ya kustaafu mpira uweze kumudu kutunza familia, kwa Afrika timu hazilipi vizuri ukifananisha na ulaya ndo mana tunashindwa kuwabakisha wachezaji wetu wazuri.

“Kwa kutokuwa na wachezaji wazuri inapelekea ligi zetu kutotazamwa sana hii ikatufanya tuje na wazo la kuanzisha Africa Super League ili kuinua timu zetu kiuchumi na kupata wachezaji wazuri kukuza ligi zetu,” .

Bingwa wa michuano ya Africa Super League atapata kitita cha dola za kimarekani milioni 11.5 ambayo ni sawa na zaidi ya billioni 27 za kitanzania, huku timu 24 zitakazo shiriki watapatiwa dola za kimarekani milioni 3.5 kila mmoja ambayo ni zaidi ya bilioni 8 za kitanzania kwa ajili ya usajili, malazi, chakula, usafiri na mengineyo.

Hawakuishia hapo pia kila nchi mwanachama wa CAF atapata dola za kimarekani milioni moja ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 2 za kitanzania kwa ajili ya kuendeleza na kukuza soka nchini mwao.

Mashindano hayo yamepitishwa na Raisi wa FIFA, Giovani Vincenzo Infantino ambaye pia alikuwepo katika huo mkutano ambapo amesema “Nina furaha kuwepo nanyi leo siku ya leo, leo ni siku ya kipekee sana kwakuwa Afrika inapiga hatua kubwa katika mpira wa miguu , Super League ni kitu kikubwa sana kwa soka la Afrika na nitakuwa na furaha nikiweza kuhudhuria mechi za CAF Super League.

Previous articleVIDEO:MAKI AZUNGUMZIA KUHUSU AISHI MANULA,BOCCO ATOA NENO
Next articleMAPEMA TU HAMTAAMINI NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI