AZAMKA KUNOGESHWA NA RAYVANNY

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa tamasha la AZAMKA ambalo ni maalumu kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji wao wapya ni maalumu kwa ajili ya mashabiki.

Kesho Agosti 14 Azam FC inatarajiwa kufanya tamasha lao la kipekee ambapo waandaaji watakuwa ni mashabiki wenyewe kwenye mipango kazi yote.

Ofisa Habari wa Azam FC,Zakaria Thabit amesema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuwa tofauti na kuwapa uhuru mashabiki wao kufanya kile ambacho wanakipenda.

“Tunakuja na AZAMKA hii itaandaliwa na mashabiki wenyewe tunataka kuona kwamba kila shabiki anaweza kushiriki na kufanya kile ambacho anakipenda nah ii ni maalumu kwa ajili yao.

“Mbali na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Zanaco,mashabiki wenyewe wataunda timu zao na kushindana wenyewe kwa wenyewe na pia kutakuwa na burudani kutoka kwa Rayvany,” amesema.

Rayvany ametunga wimo maalumu wa Azam FC kwa ajili ya tamasha la AZAMKA ambalo litafanyika kesho Uwanja wa Azam Complex.