Home Sports RASMI YANGA WAMTAKIA KILA LA KHERI BUMBULI

RASMI YANGA WAMTAKIA KILA LA KHERI BUMBULI

UONGOZI wa Yanga umemtakia kila la kheri Hassan Bumbuli ambaye alikuwa ni Ofisa Habari wa timu hiyo.

Taarifa rasmi ambayo imetolewa na Yanga imeeleza kuwa mkataba wa Hassan Bumbuli umekwisha hivyo hataongezewa mkataba mwingine.

Bumbuli alikuwa ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Taarifa hiyo imeeleza hivi:-Ndugu Bumbuli amamaliza mkataba wake wa kuitumikia Yanga hivyo uongozi unamshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kuitumikia Yanga na tunamtakia kila la kheri kwenye maisha yake mapya nje ya Klabu ya Yanga,”.

Previous articleDABI YAO YA KWANZA MASTAA HAWA WA SIMBA
Next articleMAPILATO YANGA V SIMBA HAWA HAPA