YANGA KIMATAIFA KUANZA NA ZALAN FC

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika watamenyana na Zalan FC.

Droo hiyo imepangwa leo Agosti 9 makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika, (CAF) nchini Misri.

Mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 9-11 ambapo Yanga itaanzia ugenini.

Mshindi wa mchezo huo ana kibarua cha kusaka ushindi kwa mshindi kati ya mchezo wa Al Ahly Tripoli ya Libya ama St George ya Ethiopia.

Ikumbukwe kwamba St George Agosti 8 ilikuwa Tanzania na ilicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Simba na ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.

Hivyo Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ana kazi ya kuweza kushinda kwenye mechi hizo za kimataifa.