KESHO Agosti 10,2022 mkutano mkuu wa CAF unatarajiwa kufanyika Arusha,mahali ambapo upo mlima Kilimanjaro ambao ni namba moja kwa urefu Afrika.
Mkutano huo ni wa 44 unatarajiwa kufanyika mapema asubuhi ya kesho hapo Arusha.
Wiki hii Arusha itajumuisha nchi 51 ambazo zitashiriki mkutano huo wa 44 ambao ni mkubwa na utahudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Taarifa rasmi iliyotolewa na CAF imeeleza kuwa Mji wa Arusha ni miongoni mwa miji inayovutia kutokana na kuwa na vivutio mbambali na watu wakarimu ambao wanafurahi kuwaona watu wa michezo.
Pia wamezitaja timu kongwe Bongo ambazo ni Simba na Yanga zinazoiwakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Timu mbili ambazo zina ushindani mkubwa Simba na Yanga hizi zipo pia kwenye mashindano ya CAF hivyo kuna jambo la kuweza kujadili kuhusu mpira wetu na maendeleo,”.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Wallace Karia amesema kuwa hili ni jambo kubwa ambalo walikuwa wanahitaji kuona linatokea.
“Jambo hili ni historia naona kwamba kwa muda mrefu tulikuwa tunahitaji kuona inakuwa hivi na hatimaye wageni wengi na familia ya michezo imeweza kuwasili Tanzania hii ni fahari kwangu na kila Mtanzania,” .