YANGA YAAMBULIA KICHAPO MBELE YA VIPERS SC

 DAKIKA 90 zimekamilika na ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Yanga 0-2 Vipers SC kwenye mchezo wa kirafiki.

Mchezo wa leo ulikuwa maalumu kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji pamoja na uzi mpya wa Yanga utakaotumika msimu wa 2022/23.

Ni kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi leo Agosti 6,2022 ambapo mashabiki na wanachama wa Yanga pamoja na viongozi walijitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ambazo zilikuwepo uwanjani.

Vipers ya Uganda imepata ushindi huo kwa mabao ya Milton Kalisa dk 01 na Bright Akoni dk 63 ambaye alipachika bao hilo kwa pigo huru.

Kipindi cha kwanza Yanga ilijitahidi kuweza kusaka sare ya ushindi il ngoma ilikuwa nzito na kipindi cha pili jitihada za Yanga kuweza kuweka usawa ziligonga mwamba.

Wachezaji wapya ambao wamesajiliwa na Yanga ikiwa ni pamoja na Gael Bigirimana,Bernard Morrison,Aziz KI walipata nafasi ya kucheza mchezo wa leo.