Home Sports KOCHA WA AL AHLY ACHAGUA KUPUMZIKA

KOCHA WA AL AHLY ACHAGUA KUPUMZIKA

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Al Ahly ya Misri, Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini amesema baada ya kutumika akiwa kocha kwa miaka 21, sasa ameamua kupumzika ili kufanya mambo mengine nje ya ukocha.

Pitso amesema hayo leo , Agosti 5, 2022 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam baada ya kukaribishwa na Klabu ya Yanga katika tamasha la Kilele cha Wiki ya Wananchi litakalofanyika kesho katika Uwanja wa Mkapa.

“Nikiwa kocha kutoka Afrika nimefanya makubwa kwenye soka la Afrika na nina amini Afrika tuna nafasi ya kufanya zaidi ya nilichokifanya kwenye soka kukuza mpira wetu Ulimwenguni kote.

“Nilikuwa Uwanjani kila siku na mechi za mashindano zikiwa kila baada ya siku 3 na nilikuwa nasafiri sana, sasa nimeamua kupumzika na mapumziko yangu nayatumia kushiriki na Yanga katika Wiki ya Wananchi,” amesema Pitso.

Previous articleYANGA INAHTAJI MATAJI MATATU,KUANZA NA SIMBA
Next articleLEO NI BYUTIBYUTI,SIMBA YAMSHUSHA MSERBIA