Home Sports GEITA GOLD WASHUSHA MASHINE MPYA NNE

GEITA GOLD WASHUSHA MASHINE MPYA NNE

 KLABU ya Geita Gold imetangaza kumsajili mlinzi Shawn Oduro raia wa Ghana kwa mkataba wa miaka miwili na kufanya iwe imeshusha mashine mpya za kazi nne.

Hizo ni jitihada za kukifanyia marekebisho kikosi hicho kwa ajili ya mikikimikiki ya ligi na mashindano ya CAF.

Geita Gold inayonolewa na Kocha Mkuu,Felix Minziro itashiriki mashindano ya kimataifa baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya nne msimu wa 2021/22.

 Huu ni usajili wa nne wa wachimba madini hao baada ya George Wawa kutoka Dodoma Jiji, Hussein Kazi (Polisi TZ) na Mlinda mlango Arakaza MacAthur kutoka Burundi.

Nyota huyo ambaye anakuwa usajili wa pili wa Kimataifa ametua klabuni hapo kuziba pengo lililoachwa na Mkongwe Juma Nyosso aliyetimkia Ihefu ya Jijini Mbeya.

Previous articleMWAIKIMBA ASIMULIA ALIVYOLAMBA M 58 ZA M-BET TANZANIA
Next articleBEKI BORA NDANI YA SIMBA ATAMBULISHA SINGIDA BIG STARS