KIUNGO Mnigeria,Nelson Okwa aliyekuwa anakipiga ndani ya kikosi cha Rivers United uhakika ni mali ya Simba hivyo atakuwa ni miongoni mwa wale ambao watanogesha Simba Day.
Nyota huyo alikuwa kwenye mazungumzo ya mwisho na mabosi wa Simba ambao walikuwa wakihitaji kuweza kuinasa saini yake.
Kiungo huyo ni raia wa Nigeria anakuwa mchezaji wa kwanza ndani ya Simba kutambulishwa usiku mnene ambao ilikuwa ni saa 5 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na kati.
Nyota huyo alitua usiku wa kuamkia Jumatano na ametambulishwa usiku wa kuamkia Alhamisi.
Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa bado wanaendelea na usajili na wanafanya kazi kubwa kuboresha kikosi.
“Bado tunaendelea na usajili hivyo mashabiki na wanachama wa Simba wasiwe na mashaka kuhusu hili tutafanya vizuri,” .