LEO Julai 28,2022 Yanga imezindua uzi mpya ambao unatarajiwa kutumika kwa msimu wa 2022/23.
Kwa mujibu wa Rais wa Yanga,Injinia Hersi Said amesema kuwa uzi huo kwa sasa unapatikana Tanzania nzima.
“Jezi yetu mpya ambayo tumeizindua kwa sasa inapatikana kila sehemu kwa wale wa Dodoma wasiwe na mashaka uzi wetu tayari umefika kila sehemu Watanzania wote mahali ambapo yapo maduka ya GSM.
“Bei rasmi ya jezi ni Shilingi 35,000,kuna utaratibu ambao upo kwa kupitia matawi na hiyo itafanya tuweze kufanikiwa malengo yetu,” .
Mbunifu wa uzi huo mpya ni Sheria Ngowi ameeleza kuwa kuna nembo za kila mahali ambazo zinaiwakilisha Tanzania kwenye uzi huo ikiwa ni pamoja na Mlima Kilimanjaro,Ngome Kongwe.