ZORAN Maki, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mchezo wake aliopoteza nchini Misri unampa mwanga mpana wa kutambua ubora wa kikosi chake.
Maki alishuhudia vijana wake wakinyooshwa kwa kupoteza kwenye mchezo wa tatu wa kirafiki uliochezwa nchini Misri ambapo ni mabao 2-0 walifungwa dhidi ya Haras El Hodoud
Katika mchezo wa kwanza waliambulia sare na ule wa pili walishinda huku mchezo wa tatu wakiambulia kichapo kwa kushindwa kufurukuta ugenini.
Maki Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa huo ulikuwa ni mchezo uliompa mwanga wa kujua kikosi chake.
“Tunajua kwamba mchezo wetu tumepoteza lakini haina maana kwamba hatuna uwezo hapana tunaweza na kila kitu kinawezekana kwa kuwa ni mwanzo mzuri,” amesema.