RAIS wa Senegal Macky Sall amempongeza mshambuliaji wa Simba raia wa Senegal Pape Ousmane Sakho kwa kutwaa tuzo ya bao bora la mashindano ya CAF.
Rais Sall amempongeza Sakho sambamba na wachezaji wengine wa Taifa hilo akiwemo mshambuliaji wa Klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani Sadio Mane, Golikipa wa Chelsea Edouard Mendy na mchezaji kinda Pape Matar Sarr pamoja na kocha wa Timu ya Taifa ya Senegal Aliou Cisse.
Rais Sall kupitia ukurasa wa akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram ameandika:“Ni mavuno makubwa kama nini kwa soka la Senegal kwenye #cafawards2022! Kwa ujasiri wako na vyeo vyako mpendwa Kocha @alioucisse.off, @sadiomaneoffiel, @pape_matar_sarr_15, Pape Ousmane Sakho na uteuzi, umeonyesha kwa mara nyingine tena kwamba Senegal ni taifa zuri la soka linaloheshimika.
Katika Tuzo hizo zilizotolewa na CAF jijini Rabat nchini Morocco Sadio Mane raia wa Senegal alitwaa tuzo ya mchezaji bora barani Afrika huku kocha wa Timu ya Taifa ya Senegal Aliou Cisse akifanikiwa kuchukua tuzo ya Kocha Bora wa mwaka.