HASSAN Kessy beki wa zamani wa Yanga na Simba ambaye msimu wa 2021/22 alikuwa ni mali ya KMC anatajwa kumalizana na mabosi wa Ruvu Shooting.
Kessy atajiunga na Ruvu Shooting akiwa ni mchezaji huru baada ya KMC kuweza kumshukuru kwa mchango wake ambao aliweza kuutoa kwa msimu uliopita.
Ofisa Habari wa KMC,Christina Mwagala amesema kuwa suala la Kessy wao wameshamalizana naye labda kwa wahusika wenyewe.
“Kuhusu Kessy,(Hassan) sisi tumeshamalizana naye tayari sijui labda kwa wahusika wenyewe ambao wanamhitaji,” .
Ikumbukwe kwamba Julai 20,KMC walimuaga rasmi beki huyo ambaye aliwahi kucheza Nkana FC.
Kwa upande wa Ruvu Shooting,Ofisa Habari Masau Bwire amesema kuwa mipango ikiwa tayari kila kitu kitawekwa wazi.