OFISA Habari wa Yanga, Haji Manara amepewa adhabu ya kufungiwa miaka miwili leo Julai 21.
Adhabu hiyo imetokana na makosa ambayo amekutwa nayo kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania.
Mbali na kufungiwa miaka miwili pia Manara amepewa adhabu ya kutoa faini ya shilingi milioni 20.
Baada ya adhabu hiyo,Haji Manara ametoa kauli ya kwanza baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutojihusisha na soka kwa miaka miwili ameandika haya;
“Iwe ni jambo la kheri au shari, neno langu kuu ni kumshukuru muumba mbingu na ardhi kwa neno moja kubwa na lenye maana pana sana. AL-HAMDULILLAH,”