UWANJA WA SINGIDA NI LITI,KAMBI ARUSHA

SINGIDA Big Stars kwa msimu wa 2022/23 imeweka kambi yake Arusha ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuanza Agosti.

Timu hiyo kwa sasa inaendelea kufanya maboresho kwa kuwatambulisha wachezaji wapya ambao imewapa madili mapya.

Ikumbukwe kwamba awali ilikuwa inaitwa DTB wakati huo ilipokuwa inashiriki Championship na kwa sasa imebadili jina na inaitwa Singida Big Stars.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya Singida Big Stars,Hussein Massanza amesema kuwa kambi inaendelea vizuri.

“Kambi inaendelea vema na tumechagua Arusha kwa kuwa mashabiki wetu wapo Arusha pia na ni sehemu tulivu ambayo imetulia kwa upande wa hali ya hewa na uwepo wa miundombinu bora,”.

Miongoni mwa wachezaji ambao wametambulishwa ndani ya Singida Big Stars ambayo itatumia Uwanja wa Liti kwa mechi za nyumbani ni pamoja na Said Ndemla,Paul Godfrey,Yassin Mustapha,Metacha Mnata na Benedict Haule wote wakiwa ni wazawa.