ROBERTSON ANAAMINI NUNEZ ATAKUWA MSAADA

 BEKI wa Liverpool,Andy Robertson ameweka wazi kuwa ingizo jipya ndani ya kikosi hicho Darwin Nunez utaleta mabadiliko kutokana na uwezo wake.

Ni pauni milioni 85 zimetumika na Liverpool kuipata saini ya Nunez mwenye miaka 23 ambaye ametoka Klabu ya Benfica,mwezi uliopita.

Nyota huyo alishindwa kuonyesha makeke kwenye mchezo wake wa kwanza wa kirafiki wakati timu ya Liverpool iliponyooshwa kwa mabao 4-0 dhidi ya Manchester United.

Raia huyo wa Uruguay alishambuliwa na mashabiki mtandaoni ambapo walisema kuwa hana uwezo kwa kuwa alikosa nafasi ya kufunga alipokuwa karibu na lango.

“Tunatakiwa kumuacha azoee,lakini anaonekana yuko vizuri mazoezini.Wabrazili na wengine ambao wanaongea lugha yake wamemsaidia sana.Ni mchezaji mzuri kama akionyesha kiwango chake, (cha mazoezini) atakuwa mchezaji mzuri,”.