MKAZI WA MANYARA AMESHINDA SH:106,809,410 ZA M BET

MKAZI wa Mkoa wa Manyara, Maraba Masheku, ameshinda Sh.106, 809, 410 baada ya kutabiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali za soka duniani kupitia droo ya M-Bet Tanzania ya Perfect 12.

Masheku ambaye ni shabiki wa Simba Sports Club na Chelsea amesema haikuwa kazi rahisi kwake kushinda kiasi hicho cha fedha kutokana na ugumu wa kutabiri baadhi ya timu zilizokuwa zikicheza.

Amesema mechi iliyompa wakati mgumu ni kati ya Netherland na Sweden katika mashindano ya Euro ya Wanawake, lakini alifanikiwa kutabiri matokeo sahihi. Kwa mujibu wa Masheku, timu hizo mbili zote ni nzuri na ilikuwa vigumu kutabiri matokeo yoyote kwani uwezo wao unalingana.

 “Nilikuwa njia panda kutabiri matokeo, hata hivyo, nilitumia uzoefu wangu katika kubashiri mechi na kutabiri matokeo kwa usahihi.

“Nimefurahi kuwa mshindi wa kwanza wa droo ya Perfect 12 baada ya M-Bet Tanzania kusaini mkataba wa miaka mitano na timu yangu ya Simba. Ni historia kwangu na kumbukumbu ambayo sitaisahau,” amesema Masheku.

Amesema fedha hizo atazitumia kuboresha biashara yake kwa kuongeza mtaji na vilevile kupanua mtandao wake katika soko.

“Mimi ni mjasiriamali, nina ujuzi wa kuanzisha biashara. Kwa hivyo najua jinsi ya kutumia pesa katika kuanzisha uwekezaji mdogo. Ninapaswa kuwa makini sana na jambo hilo kwa sababu unahitaji kuchambua aina ya biashara, manufaa yake na changamoto kabla ya kuamua chochote,” amesema.

Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi amesema Masheku anaungana na washindi wengine wa droo ya Perfect 12 waliofanikiwa kubadili maisha yao baada ya kujishindia mamilioni ya fedha.

Mushi pia amewataka Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 kuendelea kuweka dau lao kwa M-Bet ili kujishindia mamilioni ya fedha.