Home Uncategorized USAJILI UNAZINGATIA RIPOTI YA BENCHI LA UFUNDI?

USAJILI UNAZINGATIA RIPOTI YA BENCHI LA UFUNDI?

WAKATI timu mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara zikiwa zinafanya usajili wa wachezaji wao mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kuna mambo ngoja tuwakumbushe.

Kwanza kabisa ni kuhusu usajili ambao unaedelea kwa sasa lakini pia ni katika maandalizi yao mzuri kuelekea katika michuano ya kimataifa.

Kwa msimu ujao Yanga,Simba,Azam FC na Geita Gold zitashiriki michuano hiyo jambo ambalo ni wazi kwa timu hizo zitahitaji maandalizi ya kutusha ili waweze kufanya vizuri zaidi.

Jambo kubwa kwao ni kuhakikisha kwanza wanafanya usajili wa wachezaji wa maana na wenye uwezo mkubwa wa kuzipa mafanikio timu hizo katika michuano hiyo migumu ya kimataifa na sio vinginevyo.

Lakini kama timu hizo zitafanya usajili wa maonyesho na sio kwa ajili ya mahitaji ya timu basi tusitarajie kuona makubwa kutoka kwao.

Msimu huu katika masuala ya usajili tayari Simba,Yanga na Azam zimeonekana kuanza kufanya vurugu kwa kusajili baadhi ya wachezaji wengi kutoka nje lakini bado hatuna majibu kuwa je usajili huo utawafikisha mbali katika michuano hiyo.

Kuna kazi kubwa sana ya kufanya licha ya usajili na changamoto kubwa ambayo imeonekana kwa siku hizi za karibuni ambayo ni wachezaji wapya kushindwa kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza.

Shida hiyo imekuwa na tafsri tofauti ya kwanza ikiwa je wale wachezaji wakigeni ambao watapewa nafasi ya kucheza wakishindwa kufanya vizuri ama wakishindwa kuwa chaguo la kocha.

Kabla ya yote tukianza kuukumbuka msimu wa mwaka  2021/22 ambao ulikuwa ni msimu uliopita wa haswa katika michuano ya kimataifa tulishuhudia timu ambazo zilishiriki katika michuano hiyo zikishindwa kufika katika hatua ya makundi.

Walikuwa ni Simba na Yanga ambapo Yanga wao walitolewa na Rivers United ya Nigeria katika hatua ya awali kabisa huku Simba wao walitolewa katika hatua ya pili ya mtoano dhidi ya Jwaneng Galaxy ya nchini Botswana.

Ukiangalia sababu kubwa ilikuwa ni maandalizi ya timu zote kushindwa kujiandaa mapema katika maandalizi yao ya msimu uliopita au tunaweza kusema kuwa timu hizo zilikosa Pre Season nzuri ambazo zingeweza kuwafanya waweze kufika mbali.

Maandalizi hayakuwa mazuri yakihusisha pia maingizo mapya yaani wachezaji wapya ambao waliwasajili wengine kushindwa kuanza mapema maandalizi na timu na kuzoea mazingira jambo ambalo lilizifanya timu hizo kukosa muunganiko mzuri na kujikuta wakitolewa na timu ambazo tayari zilikuwa na muunganiko mzuri.

Kwa upande mwingine kuna baadhi ya wachezaji walikosa ITC zao  ambazo ziliwafanya washindwe kucheza ingawa tayari walikuwa  sehemu ya timu jambo ambalo msimu huu tusingependa kuliona kwani tunahitaji timu zote zikifanya maandalizi mazuri mapema ili ziweze kufika mbali.

MATUMIZI ya Picha hayana uhusiano na makala haya.

Previous articleKULIA UNAPIGWA,KUSHOTO UNAPIGWA,NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI
Next articleSIMBA WAMEANZA MAZOEZI MISRI