>

SIMBA KUWEKA KAMBI MISRI,WATARUDI WANAJUA KIARABU

AHMED Ally,Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Klabu ya Simba ameweka wazi kuwa watarejea waikiwa imara baada ya kuweka ambi nchini Misri.

Kesho,kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu Zoran Maki kinatarajiwa kuweza kuelekea nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23.

Ahmed ameweka wazi kuwa watakuwa kamili kuelekea nchini Misri na wakirudi watacheza mpira mkubwa pamoja na kuitambua lugha ya kiarabu.

“Tunaenda Misri kujipanga,tukirudi hukoo tutakuwa bora sana safari yetu ni Julai 14 kurudi ni August 4 2022.

“Tutarudi tunajua kiarabu na mpira mkubwa. Ambacho tunakuja kukifanya kwa wakati ujao ni kuweza kupambana kwa hali na mali kupata matokeo chanya kwenye mechi ambazo tutacheza.

“Mchezo wetu wa kwanza ni wa Ngao ya Jamii ambao utakuwa dhidi ya watani zetu wa jadi,tayari kocha anajua hilo na anakwenda kuandaa kikosi kwa ajili ya kuwapa furaha mashabiki na wanachama,”amesema Ahmed.