SIMBA YAMTAMBULISHA RASMI KOCHA,ATOA NENO LAKE

KOCHA Mkuu wa Simba,Zoran Maki leo Julai 12,2022 ametambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Simba ambapo ameweka wazi kwamba anatambua kwenye kila nchi kuna mechi za dabi.

Leo amewasili Tanzania raia huyo wa Serbia na anatarajia kukiongoza kikosi hicho kwa muda wa mwaka mmoja ikiwa ni mkataba ambao amesaini kuwatumikia washindi hao wa pili kwenye ligi.

Mchezo wake wa kwanza utakuwa ni wa Ngao ya Jamii ambapo itakuwa dhidi ya Yanga unatarajiwa kuchezwa Agosti 13,2022, Uwanja wa Mkapa.

Kocha huyo ametambulishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba Ahmed Ally ambapo asemema kuwa amekubali kuipa mafanikio timu hiyo.

“Kila nchi ambayo nimewahi kufanya kazi kuna mechi za watani wa jadi, ili kufanya vizuri lazima kuwa na maandalizi ya kucheza mechi za aina hiyo.

“Uzoefu ambao upo nina amini kwamba tutafanya vizuri kwenye mechi ambazo tutacheza na kikubwa ni maandalizi mazuri ambayo tutafanya hilo lipo wazi,” amesema.