VIDEO:INJINIA AFAFANUA AHADI YA UWANJA ITAKAVYOTIMIZWA

INJINIA Hersi Said mgombea wa nafasi ya Urais ndani ya Yanga ameweka wazi kwamba Wanachama watakuwa na mchango mkubwa ndani ya Yanga kutokana na mchango ambao watakuwa wanatoa.

Pia amezungumzia kuhusu kufanya vizuri kwa Yanga Princess pamoja na maendeleo yajayo.

Kuhusu ahadi ya uwanja pamoja na mafanikio ya kutwaa makombe ambayo aliahidi na akafanikiwa hayo yanampa imani ya kufanikisha mengine akiwa na Arafat ambaye anaamini ni mtu sahihi kwake.

Julai 9,2022 uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.