USAJILI WA RUVU SHOOTING NI WA MKAKAKATI

 UONGOZI wa Ruvu Shooting umeweka wazi kuwa usajili wa msimu ujao utakuwa ni wa kimkakati kwa kuwa awali walikuwa wanasubiri ligi kuisha.

Ruvu ina uhakika wa kucheza ligi msimu ujao wa 2022/23 baada ya kukamilisha ligi ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 30.

Masau Bwire,Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa walisitisha mpango wa kufanya usajili kwanza ili wahakikishe wanabaki ndani ya ligi.

“Ilikuwa ngumu kuweza kuanza mkakati wa usajili hasa ukizingatia kwamba ligi ilikuwa ngumu na kila timu hitaji lake ilikuwa ni kupata pointi tatu na maandalizi yalikuwa ni makubwa kwa kuwa tumebaki tutafanya usajili wa kimkakati.

“Haina maana kwamba hatukuwa kwenye ubora hapana kuna mambo mengine yalikuwa yanatokea ila ni mpira wetu,imani yangu yatafanyiwa kazi na bodi hasa kwenye upande wa ratiba,” amesema Masau.