PAPE AWEKA REKODI,ABEBA TUZO YAKE YA FUNGA MSIMU

PAPE Sakho,mzee wa kunyunyiza staili yake ya kushangilia ameweza kuweka rekodi ya kuwa kinara wa pasi ndani ya kikosi cha Simba baada ya kumaliza na pasi za mabao 5.

Kiungo huyo raia wa Senegal kwa msimu uliomeguka wa 2021/22 ni mechi 22 alicheza na kuyeyusha dk 1,355 na katupia mabao 6.

Kahusika kwenye mabao 10 ndani ya Simba iliyokamilisha msimu ikiwa nafasi ya pili na pointi 61 baada ya kucheza mechi 30.

Msimu huu umeonekana kuwa ni mbaya zaidi kwa Simba kwa kuwa hakuna kiungo hata mmoja aliyeweza kupenya kwenye orodha ya wale wanaowania tuzo ya kiungo bora.

Kwa msimu wa 2020/21 tuzo hiyo ilikuwa mikononi mwa Clatous Chama ambaye alitoa jumla ya pasi 15 na alikuwa ni namba moja kwenye ligi ambapo msimu huu ni Relliats Lusajo wa Namungo na Abdalahaman Mussa wa Ruvu Shooring wanaongoza wakiwa na pasi za mabao 6.

Nyota huyo pia amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Simba kwa mwezi Juni ikiwa ni tuzo ya kufunga msimu kwa mwaka 2021/22.