WAKATI wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Coastal Union, Yanga itakosa huduma ya mshambuliaji wao mmoja.
Ni Yacouba Songne ambaye amekuwa nje kwa muda mrefu baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.
Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Yanga,Cedrick Kaze amesema kuwa wanatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu wapo tayari kupata ushindi.
“Kwenye mchezo wetu wachezaji wetu wote wapo tayari isipokuwa Yacouba yeye atakuwa nje kwa kuwa bado hajawa fiti kutokana na maumivu ambayo alipata kwenye mchezo.
“Ukweli ni kwamba wachezaji wanahitaji kupata ushindi na hilo linawezekana hasa kutokana na maandalizi ambayo tumefanya kuanzia tulipokuwa tukifanya maandalizi ya mchezo wetu,” amesema.
Yanga ilitinga hatua ya fainali baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.